DHAMIRA YETU
Kukuza na kuwawezesha Viongozi duniani kote
MAONO YETU
Jumuia Zilizobadilishwa Kupitia Uongozi Uliovuviwa
MAADILI YETU YA MSINGI
Umoja, Ubunifu, Uwajibikaji, Uadilifu na Ubora
Leadership Empowerment International Network (LEIN) ni Mtandao wa Kimataifa wa Uongozi wa Madhehebu na Wasio wa Kisiasa ambao lengo kuu ni kuwawezesha Viongozi wa Kikristo na Mashirika ili kuwafanya wawe na ufanisi zaidi katika masuala ya utawala na kutumikia jamii zao.
Huduma hii ili anzishwa mwaka 2012 na watu wawili walipewa maono katika mataifa mawili tofauti na katika nyakati tofauti. Isaya 1.1 Hali hii na msukumo huu Mungu akawakutanisha, katika mwaka huu wa 2012 na kushirikishana mambo hay ana kupelekea kuzalishwa chombo kinachoitwa LEARN yaani Leadership Empowerment Africa Region Network chombo hiki kikiwa na maono ya kufikia Africa na bara lake tu.
Hapo ndipo mwezi wa nane mwaka huo 2012 mataifa matatu yalipo kutana ambayo ni Burundi, Kenya na Tanzania walipo azimia kufanya kongamano la kwanza 2012 huko Bunjumbura Burundi, baada ya kuthibitisha maono haya mataifa haya matatu waliona kuwa, kwakuwa haya maono yametoka kwa Mungu waliona ni vema maono haya yawe endelevu.
Hivyo kongamano la Burundi likazaa kongamano la pili 2013 huko Kenya chini ya mataifa matatu na viongozi hawa Mchungaji Selestin Mwiburo, Dr. Bishop Makmei, Mr. Mathew Ikombe na James Sawa ambao pia iliwapa uanachama toka Sudan ya Kusini, Rwanda na Uganda.
Maono haya yaliendelea kupata nguvu sana na kupelekea kupangwa kongamano la tatu ambalo lilipangwa kufanyika Tanzania 27 – 30 August 2014 likiwa na Nchi wnachama, Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda, Sudan ya Kusini na Rwanda.
Kwa kongamano hili likawa la baraka kubwa mno na kuzaliwa mambo muhimu ya fuatayo:-
1 Kupanuka kwa maono ya kupatikana jina jipya la LEIN likwa na maana Leadership Empowerment International Network
2 Kuundwa kwa katiba ya LEIN 2014 na kutambuliwa rasmi.
3 Chombo hiki kitatambulishwa kwa viongozi wa Serikali na Taasisi za Kidini Tanzania Mkaoni Arusha.
4 Kupatikana na kutambulishwa kwa Viongozi wa Taifa, Tanzania ambo ni Rev. Philemon Mashauri, mwenyekiti wa Taifa hilo na makamu Bishop Ezra, Katibu Samuel E. Koikai.
5 Katika kongamano hili pia ilitambulishwa rasmi nchi wanachama na waliohudhuria na waliotuma maombi ya kujiunga katika huduma hii mbele ya kiongozi mkuu wa mkoa Mheshimiwa Magesa Mlongo ambae aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Jili la Arusha.
Baada ya Kongamano hili viongozi walipanga kongamano la nne ambalo lilifanyika nchini Uganda mwaka 2015 ambalo pia lilifanyika mwezi wa nane.
Na mwaka jana 2016 lilifanyika mwezi wa kumi na mbili hapa Tanzania jijini Arusha.
Last year our seats were filled very fast so don’t miss. Conference will start in
@JESUS NEWLIFE MINISTRIES (JENELIM) CHURCH HQS – MEMBLEY, OJEY ALONG RUIRU BYPASS, KENYA From 11th December to 14th December 2025
Kukuza na kuwawezesha Viongozi duniani kote
Jumuia Zilizobadilishwa Kupitia Uongozi Uliovuviwa
Umoja, Ubunifu, Uwajibikaji, Uadilifu na Ubora
Kituo cha JENELIM, Membley – Ruiru, karibu na Bypass, Kenya
+254 720 709 625
P.O. Box 18242 – 00100, Nairobi.
connect@leinforum.org